Ni Salama

Akili za mwanadamu zingekuwaje kama tusingepitia dhambi, ungekuwa wapi sasa?

Episode Summary

Mwanzo 41:33‭-‬36 “Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa.”

Episode Notes

Jana tuliangalia kikwazo cha kwanza ni AKILI KUFUNGWA NA SHETANI na tukaangalia kwenye kile kitabu cha Luka 8:26 - 39 tukaangalia kwa undani pamoja na mistari mingine na maelezo kwa undani.

Saa nyingine huwa nawaza sana namna akili ya mwanadamu ilivyo na ambavyo inafanya mambo makubwa je kama tusingepita kwenye dhambi ingekuwaje? Kwa sababu vitu vingi vimebuniwa na akili ya mwanadamu ambayo iko kwenye dhambi na ina kiwango cha kufanya kitu ilichokifanya, sasa fikiria kama asingekuwa na dhambi ingefanya vikubwa kiasi gani? Sijasoma kwenye Biblia, lakini najaribu kufikiria kuwa kama tukifika mbinguni halafu Mungu atatuonyesha tumetumia kiwango gani cha akili zetu alizotupa na tukajikuta tumetumia kiasi kidogo sana mfano ¼, au 5% au 10% na asilimia iliyobaki akatuonyesha kulikuwa na kitu gani .Pia hiyo akili ambayo haijatumika je tungeitumia tungekuwa na maisha ya aina gani. Nakuambia watu wengi wangekata rufaa ya kurudi duniani kwa sababu ndani yake wangegundua kuwa kuna vitu vikubwa sana.

Tukiangalia mfano wa Yusufu mtoto wa mzee Yakobo kwenye Mwanzo 41, aliitwa ofisini kwa Farao kutafsiri ndoto ya Farao aliyoiota usiku na kurudia mara mbili. Mara ya kwanza Farao aliota ng'ombe wanono saba halafu wakaja wengine waliokonda kutoka kwenye mto. Wale waliokonda wakawala wale wenye afya na hata baada ya kuwala wakabaki wamekonda vile vile, akaamka; akalala na kuota ndoto nyingine akaona masuke na asubuhi yake akatafuta msaada wa tafsiri kila kona kwa waganga, wachawi na wenye hekima ili wamsaidie.

Mpaka mfanyakazi wake akaeleza alivyokutana na Yusufu jela na namna alivyo weza kuwatafsiria ndoto zao. Baada ya kusikia habari ya Yusufu ndipo Farao akaagizwa Yusufu aitwe mbele zake.Yusufu alipopewa taarifa za kuitwa kwa Farao tunona akamtafsiria Farao ndoto zake na kumweleza juu ya ujio wa miaka 7 ya chakula na unono. Baada ya pale Farao akata kujua zaidi miaka 7 ya njaa. Aliambiwa hiyo njaa itakuwa kubwa mno kiasi ambacho miaka 7 ya unono itaonekana kama haikuwepo ndio maana aliona ng'ombe waliokonda wakiwala walionona. Baada ya kuwala wale ng’ombe , wale waliokonda hawakunenepa ili kuonyesha kuwa kipindi cha njaa kitakuwa kibaya sana.

Yusufu alipomaliza kumtafsiria Farao ndoto alimwelezea kitu cha kufanya kwa sababu alikuwa anajiandaa kurudi jela. Alimwambia Farao “tafuta mtu mwenye akili na hekima umweke kwenye nafasi afanye yafuatayo